Tuesday, 15 January 2013

YA SHONZA NA CHADEMA LEO HII

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) Juliana Shonza

MAKAMU Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) Juliana Shonza ametoa shutuma nzito kwa viongozi wa ngazi za juu katika chama hicho akieleza kuwa wana lengo la kuendekeza uongozi wa kikanda jambo ambalo ni hatari kwa ukuaji wa demokrasia nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, Shonza amemtupia mawe Mwenyekiti wa Bavicha Taifa John Heche  akidai kuwa anakusudia kumburuza Mahakamani kwa kumkashifu kuwa yeye ni msaliti jambo lililomchafulia jina lake kwa jamii ya watanzania.

"Hapa mimi naongea kama Makamu mwenyekiti wa Bavicha kwani hadi leo hii sijapata barua yeyote inayoelezea kuwa mimi nimesimamishwa uongozi na uanachama chadema"alisema Shonza.

"ni jambo la kusikitisha sana kuona watu wakikiuka katiba na kanuni za chama kwa lengo la kuharibu  sifa ya mtu, ninakusudia kukutana na wakili wangu ili nipate muongozo wa kufungua kesi dhidi ya Heche,"amesema Shonza.

Amesema uamuzi uliofanya na wale wanaojiita kuwa ni wanakamati tendaji Chadema ulikiuka katiba lakini pia walitoa maamuzi pasipo kunishirikisha, kunisikia maoni yangu badala yake nikasikia tu kwenye vyombo vya habari kwamba nimefukuzwa.

Amesema chanzo cha yeye kupingwa na kuonekana mtu asiye faa ni kutetea maslahi ya chama hasa kwenye upande wa matumizi mabaya ya fedha, akitolea mfano kuwa Katibu wa chama hicho Dk Wilbrod Slaa alijikopesha pesa kiasi cha Sh140milioni ambazo hadi hivi leo hajazilipa.

Amesema sambamba na hilo Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho Freeman Mbowe amekuwa akitoa kauli zinazokigharimu chama kwa kiasi kikubwa, akifafanua kuwa badala ya yeye kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa ndani ya chadema hakuna  makundi yeye amekuwa akichangia kuyastawisha.

Amesema ameamua kuita vyombo vya habari kuvieleza kwani ameona ndiyo njia iliyotumiwa na chama hicho kufikisha ujumbe wa yeye kufukuzwa akiwa na wenzake kutoka Mbeya.

"Tuliofukuzwa ni sisi wa ukanda wa nyanda za juu kusini, lakini kwa wenzetu wa kanda za juu Kaskazini imekuwa nafuu kwao, huu si uongozi, chama kinaonekana kuwa kina mlengo wa kutawala kikanda, amesema Shonza"

CHANZ0; http://www.habarimpya.com/

Reactions:

0 comments:

Post a Comment