Wednesday, 26 December 2012

MAPENZI YA LULU NA KANUMBA YALIVYOKUWA
UHUSIANO wa kimapenzi baina ya msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kama (Lulu) ambaye anadaiwa kumuua bila kukusudia msanii mwenzake Steven Kanumba yamewekwa wazi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya msanii huyo kukiri kuwa alikuwa na uhusiano na Kanumba.

Upande wa serikali  ulisoma maelezo ya mashahidi tisa wanaotarajia kutoa ushahidi kwenye kesi hiyo pamoja na maelezo ya onyo ya Lulu aliyoyatoa kituo cha polisi Oysterbay ambayo ni moja ya vielelezo vitakavyowasilishwa mahakamani wakati kesi itakapoanza kusikilizwa rasmi katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

Tovuti hii itaendelea kuwaletea mwenendo mzima wa kesi hiyo uliogawanyika katika sehemu kuu tatu, iliyoisomwa kwa saa 1:30 na  wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro.

Akisoma maelezo hayo mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando, wakili huyo wa Serikali, alidai kuwa Lulu alitoa maelezo hayo Aprili 7 mwaka huu katika kituo cha polisi Oysterbay mbele ya Askari wa kituo hicho Ditektive Sajent Renatus.

Wakili wa serikali,Shadrack Kimaro alidai kuwa, Lulu alizaliwa mwaka 1994 na kwamba alimaliza kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Midway na baada ya hapo aliendelea na shughuli za sanaa ambazo alizianza tangu mwaka 2000.

Wakili huyo alidai kuwa Lulu alifahamiana na Kanumba kwa muda wa miaka 10, wakifanya kazi za sanaa na Januari mwaka huu ndipo  walipoanza rasmi mahusiano ya kimapenzi. Wakili huyo alidai kuwa katika mahusiano yao ya kimapenzi hawakuwahi kuishi pamoja, isipokuwa Lulu alikuwa akienda anapojisikia na mara kadhaa alikuwa akilala.

Wakili huyo alidai kuwa katika kipindi cha miezi minne ya mahusiano yao walikuwa wakigombana mara chache lakini  sababu kubwa ilikuwa ni wivu wa mapenzi kwa sababu wote walikuwa hawaaminiani.

Pia wakili huyo alidai kuwa Aprili 5 mwaka huu Kanumba na Lulu walitumiana ujumbemfupi wa simu. Itaendelea kwa hisani ya Habarimpya.com

Reactions:

0 comments:

Post a Comment