Tuesday, 12 June 2012

MWAKALEBELA KURUDI TENA IRINGA MJINI KWA KUPITIA CCM?

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa anayekumbukwa sanaa kwa ucheshi wake, Mohamed Abdulaziz akimsalimia Frederick Mwakalebela aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Taarifa zisizo rasmi zinadai kwamba Mwakalebela ameanza kujipanga kuwania ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015.

Mwakalebela anaongeza idadi ya wana CCM wanaotajwa kujiandaa kwa ajili ya kiny'ang'anyiro hicho, wengine ni Jesca Msambatavangu (Diwani wa Kata ya Miyomboni mjini Iringa) na Ritta Kabati Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM)

Reactions:

0 comments:

Post a Comment